-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Mboga ya karoti na nazi, ni mboga tamu na yenye afya ambayo hupikwa kwa kumia karoti, dengu, limao, viungo, viazi mviringo, pamoja na nazi. Mboga hii yaweza kuliwa pamoja na mlo wowote wa jioni, kama vile wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya karoti na nazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, dengu, mbegu za giligilani, chumvi, karoti, viazi mviringo, pamoja na maji, halafu weka moto mkubwa, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4.
Punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uendelee kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona viazi vimeiva, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka ndani ya hilo kontena, limao pamoja na nazi, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review