-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Mboga ya kauliflawa, karoti na maharage machanga, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia kauliflawa, karoti, maharage machanga, vitunguu maji, pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali wa binzari ya manjano au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kauliflawa, karoti na maharage machanga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za kisibiti, vitunguu maji, pamoja na kijiko 1 cha chakula cha tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka kijiko 1 cha chakula cha tangawizi iliyobaki pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka mbegu za giligilani pamoja na binzari ya manjano, kisha koroga vizuri.
Weka vikombe vya mboga mchanganyiko pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mboga hizo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mboga zimeiva.
Weka white vinegar pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review