-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Mboga ya kauliflawa, viazi na njegere, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia kauliflawa, viazi mviringo, pilipili hoho, njegere, pamoja na viungo mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kauliflawa, viazi na njegere.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, tangawizi, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, viazi, kauliflawa, njegre, pamoja na vijiko 2 vya chakula vya maji, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 25, au hadi utakapo ona viazi vimeiva.
Weka pilipili hoho, majani ya giligilani, pamoja na mango powder, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review