-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 40
-
Walaji4
Mboga ya kauliflawa, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia kauliflawa, viazi mviringo, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali wa binzari ya manjano au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kauliflawa.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye ½ kijiko cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi mviringo kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa viazi hivyo kwenye sufuria na uviweke pembeni kwenye kontena.
Weka ½ kijiko cha chakula cha mafuta ya kupikia yaliyobaki, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kauliflawa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka viazi mviringo ulivyo vikaanga, kisha koroga vizuri.
Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka tangawizi, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 25, au hadi utakapo ona viazi na kauliflawa vimeiva na kuwa laini.
Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review