-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Mboga ya njegere na viazi, ni mboga ambayo hupikwa kwa kutumia njegere zilizo chemshwa, viazi mviringo, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya njegere na viazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, viazi mviringo, pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka njegere, mbegu za giligilani, majani ya mvuje, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona njegere zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mchanganyiko huo kwenye sufuria na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka nyanya kwenye sufuria hilo hilo, kisha pika huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva. Epua nyanya hizo na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa viazi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review