-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Mboga ya njegere na vitunguu, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia njegere, vitunguu maji, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga ya njegere na vitunguu.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, tangawizi, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na njegere, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka.
Weka mango powder, limao, pamoja na garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review