Jarida la Mapishi

Mboga ya pilipili hoho na njegere

Mboga ya pilipili hoho na njegere | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Mboga ya pilipili hoho na njegere, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia pilipili hoho, vitunguu maji, nyanya, njegere, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya pilipili hoho na njegere.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba, majani ya mvuje, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka nyanya, pilipili hoho, njegere, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step3

    Weka mbegu za giligilani, mango powder, binzari ya manjano, pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step4

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.