Jarida la Mapishi

Mboga ya spinachi na viazi

Mboga ya spinachi na viazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Mboga ya spinachi na viazi, ni mboga rahisi kupika ambayo hupikwa kwa kutumia spinachi, viazi mviringo, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au ugali.  Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya spinachi na viazi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, spinachi, viazi, maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na maji yamekaribia kukauka.

    Step3

    Koroga vizuri ili baadhi ya viazi viweze kuvunjika na kutengeneza rojo, kisha epua na uweke pembeni.

    Step4

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step5

    Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step7

    Weka mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa viazi na spinachi, kisha koroga vizuri.

    Step8

    Weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.