-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1
-
Walaji4
Mchuzi wa dengu, ni mchuzi mtamu na rahisi kupika, ambao hupikwa kwa kutumia mbaazi, nyanya, mtindi, pamoja na viungo mbali mbali, kama vile tangawizi. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa dengu.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka dengu ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 24. Baada ya saa 24, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na dengu peke yake.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, dengu, vikombe 4½ vya maji, baking soda, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona dengu zimeiva, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona nyanya hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka mbegu za giligilani, garam masala, binzari ya manjano, pamoja na limao halafu koroga vizuri.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye dengu.
Weka sufuria hilo lenye dengu kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha chemsha huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15.
Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review