Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kamba

Mchuzi wa kamba | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa kamba, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia kamba wabichi, white vinegar, nyanya, vitunguu maji, pamoja na viungo. Mchuzi huu wa kamba, wafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa kamba.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya mvuje, binzari nyembamba, mbegu za haradali, garam masala, chumvi, sukari, binzari ya manjano, pamoja na white vinegar, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step2

    Weka nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona nyanya hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini pamoja na majani ya mbei, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step4

    Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step5

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka mchanganyiko wa viungo uliomo kwenye kontena, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Weka nyanya ulizo zisaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step7

    Weka kamba, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona kamba wamebadilika rangi na kuwa na rangi ya pinki.

    Step8

    Weka majani ya giligilani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.