Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kuku wa kusaga

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, kuku wa kusaga, iliki, karafuu, mdalasini, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha sufuria lipate moto. Weka kwenye hilo sufuria, vitunguu maji pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona imepata moto.

    Step3

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5.

    Step4

    Ongeza moto na uweke moto wa wastani. Weka mchanganyiko wa kuku, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona nyama ya kuku imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.

    Step6

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.