Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kuku wenye korosho na mpopi

  • Maandalizi
    Saa 1
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikombe chenye maji ya moto, kisha roweka korosho mbichi pamoja mbegu za mpopi ndani ya hicho kikombe chenye maji ya moto kwa muda wa saa 1.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko wa maji ya moto, iliki, vitunguu swaumu, tagawizi, vitunguu vya kijani, majani ya giligilani, pamoja na mtindi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pilipili manga, mbegu za giligilani, garam masala, chumvi, pamoja na vipande vya nyama ya kuku, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mchanganyiko huo kwenye kikaango na uweke pembeni kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step4

    Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka mchanganyiko wa korosho ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekaribia kukauka.

    Step5

    Punguza moto na uweke moto wa wastani. Weka vipande vya nyama ya kuku vilivyomo kwenye kontena, halafu funika kikaango, kisha pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step6

    Weka heavy cream halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika kadhaa. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.