Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kuku wenye zafarani na lozi

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, Yogurt Cheese, mtindi, mafuta ya kupikia, vitunguu maji, lozi, binzari nyembamba, garam masala, tangawizi, iliki, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka vipande vya nyama ya kuku, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step3

    Chukua kikombe. Weka maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.

    Step4

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka mchanganyiko wa kuku kwenye hilo sufuria, kisha liweke kwenye jiko lenye moto mkubwa. Funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5. Kumbuka kukoroga mara 1 au 2 wakati unapika.

    Step5

    Punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funua sufuria, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva.

    Step6

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka mchanganyiko wa zafarani pamoja na majani ya minti halafu koroga vizuri. Funika sufuria, halafu pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.