-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Mchuzi wa maboga, ni mchuzi wenye ladha nzuri na rahisi kupika, ambao hupikwa kwa kutumia maboga, mbaazi, choroko, tui la nazi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa brown, mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa maboga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maboga, mbaazi, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na maji halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona maboga pamoja na mbaazi vimeiva.
Weka nazi pamoja na binzari nyembamba, halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona maji yamekaribia kukauka. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka choroko kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa maboga, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review