Jarida la Mapishi

Mchuzi wa matango

Mchuzi wa matango | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Mchuzi wa matango, ni mboga yenye ladha nzuri na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia matango, nazi, mbaazi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali mweupe au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa matango.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, mbaazi, maji, tangawizi, pamoja na majani ya mvuje, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva.

    Step3

    Weka matango halafu koroga vizuri, kisha ichemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hado utakapo ona matango yameiva.

    Step4

    Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena.

    Step5

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya nazi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje yaliyo twangwa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa matango, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.