-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Mchuzi wa mbaazi, ni chakula kitamu, chenye virutubisho na rahisi kupika, ambacho chafaa kuliwa pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa mbaazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, mbaazi, maji, chumvi, pamoja na binzari ya manjano, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva.
Weka limao na ukoroge vizuri, halafu epua na uweke kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, vitunguu maji pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka binzari nyembamba, pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka mbegu za giligilani, kisha endelea kukaanga kwa muda wa dakika 1 zaidi. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mbaazi, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review