Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nyama ya kondoo

Mchuzi wa nyama ya kondoo | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 25
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nyama ya kondoo, ni kitoweo kitamu, ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kondoo, vitunguu maji, nyanya, nazi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali au pilau. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya kondoo.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya giligilani, pamoja na majani ya mvuje, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step2

    Weka nyanya, garam masala, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na vipande vya nyama ya kondoo, kisha kaanga huku ukivigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Weka mchanganyiko ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.

    Step6

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15.

    Step7

    Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, au hadi utakapo ona nyama imeiva.

    Step8

    Mimina tui la nazi na ukoroge vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.