Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nyama ya kusaga na adesi

Mchuzi wa nyama ya kusaga na adesi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nyama ya kusaga na adesi, kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia, nyama ya kusaga, vitunguu maji, adesi, ukwaju, pamoja na viungo. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari ya manjano, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza mchuzi huu wa nyama ya kusaga na adesi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka adesi ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 1. Baada ya saa 1, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na adesi peke yake.

    Step2

    Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, mbegu za giligilani, garam masala, Tamarind Powder, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na ½ kikombe cha maji, kisha changanya hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za haradali, mbegu za uwatu, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step4

    Weka nazi, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Weka mchanganyiko wa viungo uliomo kwenye kontena dogo, nyama ya kusaga, pamoja na adesi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Weka maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step7

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona adesi zimeiva na mchuzi umekuwa mzito.

    Step8

    Weka tui la nazi pamoja na majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.