Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nyama ya kusaga na spinachi

Mchuzi wa nyama ya kusaga na spinachi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nyama ya kusaga na spinachi, kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia, nyama ya kusaga, vitunguu maji, spinachi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari ya manjano, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo ili ujifunze jinsi kupika mchuzi huu wa nyama ya kusaga na spinachi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, binzari nyembamba, nyama ya kusaga, vitunguu maji, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya mvuje, mbegu za giligilani, garam masala, mbegu za uwatu, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka spinachi pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona spinachi imenyauka.

    Step3

    Mimina tui la nazi halafu funika sufuria, kisha acha ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.