-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1 Dk. 10
-
Walaji4
Mchuzi wa nyama ya mbuzi, ni kitoweo kitamu, ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya mbuzi, vitunguu maji, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali au pilau. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya mbuzi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi pamoja na zafarani, kisha changanya vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, pilipili manga, iliki, majani ya mbei, karafuu, pamoja na binzari nyembamba, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.
Weka tangawizi, vitunguu swaumu, vipande vya nyama ya mbuzi, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vipande hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke kwa muda wa dakika 5.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona nyama imeiva.
Weka garam masala na ukoroge vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na uweke pembeni.
Weka mchanganyiko wa mtindi na zafarani, pamoja na majani ya giligilani, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review