-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1 Dk. 55
-
Walaji4
Mchuzi wa nyama ya ng’ombe, ni kitoweo chenye ladha na harufu nzuri, ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya ng’ombe, vitunguu maji, nyanya, mtindi, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya ng’ombe.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda 3 mpaka 5.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 12, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka mbegu za giligilani, garam masala, binzari nyembamba, pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka nyama pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mtindi umekauka.
Weka maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 45 mpaka 55, au hadi utakapo ona nyama imeiva na mchuzi umekuwa mzito.
Weka majani ya uwatu halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review