Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nyanya

Mchuzi wa nyanya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nyanya, ni mboga tamu iliyo sheheni ladha ya uchachu, ambayo hupikwa kwa kutumia nyanya zilizoiva, vitunguu maji, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali, mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyanya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka binzari nyembamba pamoja na mbegu za giligilani, kisha koroga vizuri.

    Step3

    Weka nyanya pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona nyanya zimekuwa rojo.

    Step4

    Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step5

    Weka pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.