-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Mchuzi wa samaki, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia samaki wabichi, vitunguu maji, tui la nazi, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa samaki.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimeiva.
Weka vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za giligilani pamoja na binzari nyembamba, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka binzari ya manjano, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye sufuria lenye vitunguu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Mimina maji pamoja na tui la nazi, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke huku ukikoroga mara kwa mara.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5.
Weka Tamarind Paste pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 1.
Weka vipande vya minofu ya samaki, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review