Jarida la Mapishi

Mchuzi wa viazi mviringo

Mchuzi wa viazi mviringo | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Mchuzi wa viazi mviringo, ni mchuzi wenye ladha nzuri na rahisi kupika, ambao hupikwa kwa kutumia, viazi mviringo, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali, mkate, au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa viazi mviringo.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo, chumvi kiasi, pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Nyunyizia binzari ya manjano, kisha changanya vizuri.

    Step5

    Chukua sufuria kubwa lenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi mviringo kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa viazi hivyo kwenye sufuria na uviweke pembeni kwenye chombo safi.

    Step6

    Weka vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia vilivyobaki, kisha acha mafuta yapate moto.

    Step7

    Weka mdalasini pamoja na iliki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde kadhaa.

    Step8

    Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step9

    Weka viazi ulivyo vikaanga pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step10

    Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga.

    Step11

    Mimina vikombe 2 vya maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na kuwa laini.

    Step12

    Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.