Jarida la Mapishi

Mchuzi wa viazi vya kukaanga

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo, chumvi kiasi, pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 10.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mtindi pamoja na vikombe 1½ vya maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step5

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi ulivyo vichemsha kwenye hicho kikaango, halafu kaanga huku ukivigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni. Ondoa viazi hivyo kwenye kikaango na uviweke pembeni kwenye kontena lenye paper towel, kisha acha vikauke mafuta.

    Step6

    Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia yaliyomo kwenye kikaango, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, iliki, mdalasini, karafuu, viazi ulivyo vikaanga, mbegu za shamari, mbegu za giligilani, tangawizi, pamoja na kijiko 1 cha chai cha chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona viungo vimeshikamana pamoja na viazi.

    Step7

    Mimina mchanganyiko wa mtindi ulio usaga, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step8

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step9

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.