Jarida la Mapishi

Mchuzi wa viazi wenye minti

Mchuzi wa viazi wenye minti | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Mchuzi wa viazi wenye minti, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo, vitunguu maji, nazi, majani ya minti, pamoja na viungo vingine. Pishi hili lafaa kula pamoja na wali wa binzari nyembamba, mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa viazi wenye minti.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo, chumvi kiasi, pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya minti, pamoja na nazi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step5

    Weka mbegu za giligilani pamoja na binzari ya manjano, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step6

    Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria binzari nyembamba pamoja na viazi mviringo, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa viazi hivyo kwenye sufuria na uviweke pembeni kwenye kontena.

    Step7

    Weka vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia yaliyobaki kwenye sufuria hilo hilo, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step8

    Weka viazi ulivyo vikaanga, ½ kijiko cha chai cha chumvi, pamoja na vikombe 3 vya maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona viazi vimekuwa laini na mchuzi umekuwa mzito.

    Step9

    Weka majani ya minti ya unga pamoja na garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.