Jarida la Mapishi

Mchuzi wa vitunguu maji

Mchuzi wa vitunguu maji | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa vitunguu maji, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia vitunguu maji, nyanya, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa vitunguu maji.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vikombe 5 vya vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka nyanya, vikombe 3 vya vitunguu maji vilivyobaki, chumvi, pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva.

    Step3

    Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step5

    Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step6

    Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 3 zaidi, au hadi utakapo ona majani hayo yamenyauka. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.