Jarida la Mapishi

Mishikaki ya maini ya kuku

Mishikaki ya maini ya kuku | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    4

Mishikaki ya maini ya kuku, ni moja ya vyakula maarufu vya mtaani katika nchi za India na Morocco. Mishikaki hii hupikwa kwa kutumia maini ya kuku, yaliyo changanywa pamoja na viungo na kisha kuchomwa kwenye jiko la kuchomea nyama. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki ya maini ya kuku.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, maini ya kuku, mtindi, tomato sauce, vitunguu maji, majani ya uwatu, mbegu za giligilani, garam masala, binzari nyembamba, mafuta ya kupikia, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na limao, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya maini ya kuku vimeenea vyema viungo.

    Step2

    Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step3

    Chukua kikaango. Weka mchanganyiko wa maini ya kuku kwenye hicho kikaango, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona maini yameiva na mchuzi umekaribia kukauka, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step5

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka vijiti vya mishikaki ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step6

    Baada ya dakika 30, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na vijiti peke yake.

    Step7

    Chukua vijiti vya mishikaki, kisha chomeka vipande vya maini ya kuku kwenye hivyo vijiti.

    Step8

    Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mishikaki juu ya jiko la kuchomea nyama, kisha choma mishikaki hiyo huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona pande zote za mishikaki hiyo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step9

    Ondoa mishikaki hiyo kwenye jiko la kuchomea nyama na uiweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.