-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Mishikaki ya mbuzi, ni mishikaki mitamu yenye ladha ya kupendeza na nyepesi kuliko ya kondoo. Nyama hii ni laini sana hata ukiipika bila kutumia mafuta ya kupikia. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki hii ya mbuzi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena kubwa. Weka vipande vya nyama ya mbuzi ndani ya hilo kontena, kisha weka pembeni.
Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, mtindi, tangawizi, vitunguu swaumu, limao, mafuta ya kupikia, mbegu za giligilani, binzari nyembamba, garam masala, pamoja na chumvi. Mimina mchanganyiko huu kwenye kontena lenye nyama ya mbuzi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya mbuzi vimeenea vyema viungo.
Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 24.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka vijiti vya mishikaki ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Baada ya dakika 30, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na vijiti peke yake.
Chukua vijiti vya mishikaki, kisha chomeka vipande vya nyama ya mbuzi kwenye hivyo vijiti.
Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mishikaki juu ya jiko la kuchomea nyama, kisha choma mishikaki hiyo huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 19, au hadi utakapo ona pande zote za mishikaki hiyo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Paka siagi kwenye mishikaki hiyo, halafu endelea kuchoma kwa muda wa dakika 1 zaidi, kisha ondoa kwenye jiko la kuchomea nyama na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review