-
MaandaliziDakika 35
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Ikiwa wewe ni mpenzi wa chocolate, basi jaribu pishi hili la mkate wa chocolate. Mkate huu wa chocolate, ni mkate rahisi sana kuupika na unaweza kuupika mkate huu kwa muda mfupi sana wa dakika 45 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, mafuta ya kupikia ya nazi, tui la nazi, mayai, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka unga wa ngano, cocoa, chumvi, baking powder na nazi iliyokunwa, changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kuchanganyia, kisha weka dark chocolate chips ndani ya huo mchanganyiko na ukoroge vizuri.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review