-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa limao, ni mkate mtamu unaopikwa kwa kutumia limao halisi lililo kamuliwa, pamoja na maganda yake yaliyokunwa, kisha kusagwa. Fuata hatua zifuatazo, ilu ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa limao.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa ngano, chumvi pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri.
Weka buttermilk, sour cream, mafuta ya kupikia, limao lililo kamuliwa, maganda ya limao uliyo yakuna, yai na thaimu, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review