-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa ndizi, ni mkate mtamu na rahisi kuandaa ambao unaweza kuandaa bila hata kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer). Unachohitaji ili kuupika mkate huu ni ndizi siagi, sukari na unga wa ngano. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa ndizi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, sukari, pamoja na siagi, kisha changanya vizuri.
Weka mayai na uendelee kuchanganya, halafu weka ndizi na buttermilk, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema.
Weka unga wa ngano ambao hauja kobolewa, cocoa powder, baking powder, unga wa ngano, chumvi na mdalasini, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review