-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji12
Mkate wa pekani kama jina lake lilivyo, ni mkate unaopikwa kwa kutumia njugu za pekani. Ukiachana na njugu za pekani, mkate huu pia huchanganywa pamoja na viungo kama vile kungumanga, ili kuufanya mkate huu uwe na ladha nzuri zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa pekani.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, ndizi mbivu, mafuta ya kupikia, pamoja na maziwa ya lozi, kisha changanya vizuri.
Weka unga wa ngano, unga wa ngano ambao hauja kobolewa, pekani, dark brown sugar, baking powder, mbegu za kitani na kungumanga, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review