-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa zucchini, ni mkate mtamu na rahisi kupika, ambao hupikwa kwa kutumia zucchini zilizo kunwa. Mkate huu wafaa sana kuliwa katika msimu wa kiangazi kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitafunio cha kawaida wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa zucchini.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, zucchini, mayai, buttermilk, mafuta ya kupikia, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka light brown sugar, unga wa ngano ambao hauja kobolewa, mbegu za kitani, chumvi na baking powder, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review