Jarida la Mapishi

Nyama ya kukaanga

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, sour cream, white vinegar, garam masala, mbegu za uwatu, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama pamoja na mchanganyiko wa viungo ulio usaga, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step3

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vipande vya nyama kwenye hicho kikaango kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Nyunyizia juu ya hivyo vipande vya nyama, majani ya uwatu pamoja na limao, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.