-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Pilau ya mahindi na njegere, ni chakula kizuri na chenye afya ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, mahindi mabichi, njegere pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya mahindi na njegere.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka binzari nyembamba, mbegu za haradali, majani ya mvuje, majani ya uwatu, majani ya minti, pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Weka njegere, mahindi, vitunguu maji, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka nyanya, majani ya giligilani, pamoja na wali mweupe halafu koroga vizuri. Funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review