Jarida la Mapishi

Pilau ya uwatu

Pilau ya uwatu | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Pilau ya uwatu, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, viazi mviringo, majani ya uwatu, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Chakula hiki chafaa kula pamoja na kinywaji cha mtindi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya uwatu.

Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika pilau ya binzari nyembamba, ambayo utaitumia katika kupika pilau hii ya uwatu.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria kiazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona kimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na kiazi peke yake, kisha acha kipoe.

    Step3

    Menya maganda ya kiazi hicho, kisha kikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka majani ya uwatu kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step5

    Weka viazi mviringo, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye chombo chenye pilau ya binzari nyembamba.

    Step6

    Nyunyizia garam masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.