Jarida la Mapishi

Pilau ya uyoga na pistachio

Pilau ya uyoga na pistachio | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1 Dk. 30
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Pilau ya uyoga na pistachio, ni pilau tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia uyoga ulio kaushwa, mchele, njugu za pistachio, vitunguu maji, pamoja na viungo. Pilau hii yafaa kula kama chakula cha mchana au cha jioni, pamoja na saladi ya vitunguu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya uyoga na pistachio.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka maji, kisha roweka uyoga ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 1. Baada ya saa 1, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na uyoga peke yake.

    Step2

    Osha uyoga kwenye maji yanayo tiririka, kisha kata katika vipande vidogo vidogo.

    Step3

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka vikombe 2⅓ vya maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, majani ya mbei, pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step5

    Weka binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step6

    Weka tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya minti, mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step7

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka lakini wali bado haujaiva.

    Step8

    Weka vipande vya uyoga, majani ya giligilani, pamoja na ½ ya njugu za pistachio, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona wali umeiva.

    Step9

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko.

    Step10

    Weka ½ ya njugu za pistachio zilizobaki pamoja na garam masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.