Jarida la Mapishi

Pilau ya vitunguu na brokoli

Pilau ya vitunguu na brokoli | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    4

Pilau ya vitunguu na brokoli, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, brokoli, vitunguu maji, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile; iliki, mdalasini, pamoja na karafuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya vitunguu na brokoli.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye vijiko 3 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, pamoja na karafuu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step3

    Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step4

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Nyunyizia sukari juu ya vitunguu maji, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa nusu ya vitunguu hivyo kwenye sufuria na uviweke pembeni kwenye kontena lenye paper towel.

    Step5

    Weka kwenye sufuria lenye vitunguu, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step7

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko.

    Step8

    Chukua sufuria dogo lenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na brokoli, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye pilau.

    Step9

    Weka vitunguu maji vilivyomo kwenye kontena juu ya hiyo pilau, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.