-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Pilau ya zafarani, ni pilau tamu na rahisi kupika ambayo hupikwa kwa kutumia mchele pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile zafarani, iliki na mdalasini. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya zafarani.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka zafarani kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu zafarani ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona zimesagika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, majani ya mbei, pamoja na iliki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka binzari nyembamba, mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele.
Weka zafarani ulizo zikaanga pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Nyunyizia garam masala, kisha koroga vizuri.
Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review