Jarida la Mapishi

Pilau ya zafarani na lozi

Pilau ya zafarani na lozi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Pilau ya zafarani na lozi, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, maziwa, lozi, pistachio, zafarani, pamoja na viungo vingine. Pilau hii yafaa kula pamoja na kitoweo cha kuku au samaki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya zafarani na lozi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka lozi kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni.

    Step3

    Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 15.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, binzari, nyembamba, iliki, pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step5

    Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele.

    Step6

    Weka chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step7

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona wali umekaribia kuiva.

    Step8

    Nyunyizia maziwa yenye zafarani juu ya huo wali, halafu funika sufuria, kisha endelea kupika wali huo kwa muda wa dakika 5 zaidi. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step9

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko.

    Step10

    Weka garam masala, lozi, pamoja na pistachio, halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.