-
MaandaliziSaa 2
-
KupikaDakika 5
-
Walaji4
Saladi ya kamba na tangawizi, ni saladi tamu na rahisi kutengeneza, ambayo hutengenezwa kwa kutumia kamba wakubwa, pilipili hoho, vitunguu maji, mboga, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile tangawizi. Saladi hii yafaa kula katika msimu wa kiangazi pamoja na chakula chochote cha mchana au cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya kamba na tangawizi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, kamba, tangawizi, vitunguu swaumu, limao, mbegu za kisibiti, chumvi, pamoja na pilipili manga, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona kamba wote wameenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka majani ya minti kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Weka mchanganyiko wa kamba, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona kamba wamebadilika rangi na kuwa na rangi ya pinki.
Chukua kontena jingine kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vikombe vya mchanganyiko wa mboga ya spinachi na mchunga, pilipili hoho, tango, pamoja na Chaat Masala, kisha changanya vizuri.
Epua sufuria lenye mchanganyiko wa kamba na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa mboga, kisha sambaza vizuri kamba hao.
Nyunyizia vitunguu vya kijani, tayari kwa kula.
Leave a Review