-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1
-
Walaji4
Saladi ya kunde, ni saladi yenye afya isiyokuwa na gluteni. Saladi hii hutengenezwa kwa kutumia kunde, vitunguu vya kijani, mtindi, nyanya, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya kunde.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka vikombe 2 vya maji, kisha roweka kunde ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 24.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, kunde, maji uliyotumia kurowekea kunde, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona maji yamekauka na kunde zimeiva, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka ndani ya hilo kontena, nyanya, vitunguu vya kijani, tangawizi, majani ya minti, pamoja na limao halafu koroga vizuri, kisha acha ipoe.
Ukiona imepoa mimina mtindi, kisha koroga tena vizuri.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye saladi.
Nyunyizia Chaat Masala, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review