Jarida la Mapishi

Saladi ya viazi vitamu

Saladi ya viazi vitamu | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    4

Saladi ya viazi vitamu, ni saladi tamu ambayo hutengenezwa kwa kutumia viazi vitamu vilivyo chemshwa, ukwaju, sukari, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya viazi vitamu.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step4

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step5

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step6

    Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, majani ya giligilani, chumvi, sukari, tangawizi, binzari nyembamba, Tamarind Paste, pamoja na viazi vitamu ulivyo vichemsha, halafu changanya vizuri, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 1, kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.