Jarida la Mapishi

Samaki wa kubanika

Samaki wa kubanika | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Samaki wa kubanika, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho huandaliwa kwa kutumia minofu ya samaki wabichi walio changanywa na viungo, limao, pamoja na heavy cream, kisha kubanikwa kwenye jiko la kuokea (oven). Waweza kula kitoweo hiki kama chakula cha mchana, pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha samaki wa kubanika.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya minofu ya samaki, binzari nyembamba, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 24.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, mafuta ya kupikia, heavy cream, limao, mbegu za haradali, pamoja na mbegu za kisibiti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena lenye samaki, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya samaki vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1.

    Step4

    Washa jiko la kubanikia, kisha acha lipate moto. Weka vipande vya minofu ya samaki ndani ya hilo jiko, kisha banika kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona upande wa juu wa vipande hivyo vya samaki umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Geuza upande wa pili wa vipande hivyo vya samaki, kisha banika kwa muda wa dakika 4 mpaka 5, au hadi utakapo ona na upande wa pili wa vipande hivyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa vipande hivyo vya samaki kwenye jiko la kubanikia na uviweke pembeni kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.