-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 2 Dk. 40
-
Walaji24
Sambusa za viazi, ni kitafunio maarufu ambacho hupikwa kwa kuchanganya viazi mviringo pamoja viungo, na kisha kukaangwa kwenye mafuta. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sambusa hizi za viazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na viazi mviringo, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka tangawizi, mbegu za giligilani, ½ kijiko cha chai cha chumvi, pamoja na garam masala, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka majani ya giligilani pamoja na mango powder, halafu endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (food processor). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vikombe 1½ vya unga wa ngano, baking powder, chumvi, baking soda, ¼ kikombe cha mafuta ya kupikia, mbegu za kisibiti, pamoja na kijiko 1 cha chai cha chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Mimina ⅓ ya kikombe cha maji taratibu wakati mashine ikiendelea kuzunguka, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umejikusanya na kuwa donge lenye umbo la mpira ambalo halishikamani na chombo. Ondoa donge hilo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uliweke kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo, kisha acha donge liumuke kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.
Chukua mafuta ya kupikia kiasi na uyapake kwenye viganja vya mikono yako. Chukua donge lililomo kwenye kontena, kisha ligawe katika madonge 12 ya maumbo ya mpira yenye uwiano unao fanana. Weka madonge hayo kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.
Chukua kibao cha kusukumia chapati. Chukua donge moja kutoka kwenye kontena na uliweke juu ya kibao cha kusukumia chapati, kisha kandamiza vizuri donge hilo kwa kutumia kiganja cha mkono wako hadi utakapo ona imekuwa bapa.
Chukua unga wa ngano na upake juu ya donge ulilo likandamiza. Chukua kifimbo cha kusukumia chapati, kisha sukuma hadi utakapopata chapati ya upana wa kati ya nchi 6 hadi 7. (Unaweza kupaka unga zaidi wakati unasukuma, ikiwa utaona donge hilo linanata)
Chukua kisu na ukate chapati hiyo katikati, kisha chukua maji na upake kwenye kingo za vipande hivyo vya chapati.
Chukua kipande kimoja cha chapati. Chukua upande mmoja wa kipande hicho cha chapati na ukunje katikati, halafu chukua na upande wa pili wa kipande hicho cha chapati na ukunje pia katikati ili kutengeneza umbo la koni. Hakikisha kingo za pande zote mbili za hiyo chapati zimekutana, kisha kandamiza kingo hizo ili ziweze kushikamana.
Fungua mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha weka ndani yake vijiko 2 hadi 3 vya chakula vya mchanganyiko wa sambusa ulio upika.
Chukua maji na upake kwenye kingo za mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha kandamiza kingo hizo, hadi utakapo ona mdomo wa sambusa umejifunga vizuri. Weka sambusa hiyo kwenye kontena safi, kisha funika vizuri kontena hilo, hadi utakapokuwa tayari kukaanga sambusa hizo. Rudia hatua ya 10 hadi ya 15 kwa madonge yaliyobaki.
Chukua kikaango kikubwa chenye vikombe 2 vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango sambusa ambazo zinatosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa sambusa hizo kutoka kwenye kikaango na uziweke kwenye kwenye chombo chenye paper towel ili zikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa sambusa nyingine zote zilizobaki.
Leave a Review