Maelezo yafuatayo yanaelezea sera ya faragha kuhusiana na taarifa za mtu za kibinafsi ambazo tunakusanya kuhusiana na wewe.
Maelezo ya dhamira
Kuna wakati, utaombwa kuwasilisha taarifa zako za kibinafsi (kwa mfano, jina na anuani ya email, nk) ili kupata au kutumia baadhi ya huduma zilizopo kwenye mtandao wetu.
Kwa kuandika maelezo yako kwenye nafasi zilizopo, unairuhusu Jarida la Mapishi kukupatia huduma ulizoziomba. Kila unapotoa maelezo yako ya kibinafsi, tutahifadhi taarifa hizo kwa kuzingatia sera hii. Huduma zetu zimekusudiwa kukupatia taarifa unazotaka kupata. Jarida la Mapishi itashughulika kulingana na sheria za sasa hivi na itadhamiria kutekeleza taratibu nzuri kabisa za sasa hivi za Internet.
Tarifa za wageni
Wakati wowote unapotembelea mtandao wa Jarida la Mapishi, kurasa unazoziona, pamoja na kitu kinachoitwa cookie, zinaingizwa kwenye kompyuta yako (angalia kipengee cha 3 kupata mengi juu ya hili). Karibu kurasa zote, kama siyo zote kabisa, zinafanya hivyo, kwa sababu cookies zinaiwezesha kampuni inayomiliki kurasa hizo kufanya vitu vingi vyenye manufaa, kama vile kujua kama kompyuta hiyo (na huenda mtumiaji wake) ametembelea ukurasa huo hapo awali. Hii inafanyika wakati mtumiaji huyo anarejea tena kwenye mtandao, kwa kuchunguza ili kuangalia na kuikuta cookie iliyoachwa hapo nyuma, wakati mtumiaji alipozuru mtandao mara ya mwisho.
Taarifa yoyote ambayo imetolewa na cookies inaweza kutusaidia kukupa wewe huduma bora na kutusaidia kuchunguza wasifa wa wageni wetu. Kwa mfano: kama ulipotembelea kurasa zetu mara ya mwisho, tuseme uliingia kwenye kurasa za elimu, basi tunaweza kukuta taarifa hizi kwenye cookie yako na kielelezo cha taarifa za elimu utakapoingia mara ya pili.
Kampuni ya Google, inakusanya data ambazo siyo za kibinafsi zinazowahusu wageni wanaozuru kurasa zetu kwa niaba yetu kwa kutumia cookies na alama ambayo imewekwa kwenye mtandao wetu. Cookies hizo na alama iliyopo kwenye mtandao vinatoa takwimu ambazo siyo za kibinafsi kuhusu ziara zilizofanywa kwenye kurasa zetu, muda uliotumika kuangalia ukurasa, njia zilizotumiwa na wageni hao kwenye mtandao, data zilizopo kwenye mipangilio ya skrini za wageni na taarifa nyingine za kawaida. Jarida la Mapishi inatumia taarifa kama hizi, na zile zilizopatikana kwenye cookies nyingine zilizotumika kwenye mtandao huo kusaidia kuboresha huduma kwa watumiaji wake.
Cookie ni nini?
Unapoingia kwenye mtandao, kompyuta yako mara moja itapewa cookie. Cookies ni faili za maandishi zinazoitambulisha kompyuta yako kwenye mtambo wetu wa mtandao unaohifahdi kumbukumbu zote (server). Cookies zenyewe hazimtambui mtumiaji, ila tu zinaitambua kompyuta iliyotumiwa. Makampuni mengi ya mtandao yanafanya hivyo wakati mtumiaji anapozuru kurasa zao ili kuweza kujua jinsi watu wanavyoingia na kutoka kwenye mtandao huo.
Cookies zenywe zinachukua kumbukumbu za maeneo ya mtandao ambayo yametembelewa na kompyuta husika, na kwa muda gani. Watumiaji wanapata fursa ya kuzifanya kompyuta kuruhusu cookies zote, kuwafahamisha wakati ambapo cookie imetolewa, au kutopokea cookies wakati wowote ule. Hili la mwisho linamaanisha kwamba huduma fulani fulani za kibinafsi hazitaweza kutolewa kwa mtumiaji huyo.
Matumizi na hifadhi ya taarifa zako za kibinafsi
Unapotoa taarifa zozote za kibinafsi kwa Jarida la Mapishi (kwa mfano, kwa ajili ya mashindano au huduma za jamii za Jarida la Mapishi (Jarida la Mapishi Community) kisheria tunawajibika kwako katika kuangalia jinsi tunavyotumia data hizo. Tunapaswa kukusanya taarifa hizo kwa haki, hii inamaanisha kwamba tunalazimika kukuelezea jinsi tutakavyotumia data hizo (angalia matangazo kwenye kurasa husika ambazo zinakufahamisha kwa nini tunaomba maelezo hayo) na kukuambia kama tunataka upeleke taarifa hizo kwa mtu mwingine yeyote yule. Kwa kawaida, taarifa zozote zile unazozitoa kwa Jarida la Mapishi zitatumika ndani ya Jarida la Mapishi na watu wake wanaotoa huduma. Kamwe hazitapelekwa kwa mtu eyote yule nje ya Hildegard Studios bila kupata idhini yako kwanza, isipokuwa tunapowajibika au tunaporuhusiwa kisheria kufichua taarifa hizo. Vile vile, kama unatuma au kupeleka maelezo yenye matusi au yasiyofaa juu ya Jarida la Mapishi au kwa Jarida la Mapishi na kama Jarida la Mapishi itaona kwamba mwenendo huo ni mbaya na/au umerudiwa, Jarida la Mapishi inaweza kutumia taarifa zozote zile zilizopatikana kuhusiana na wewe ili kukomesha mwenendo huo. Hii ni pamoja na kuwafahamisha watu wengine kama vile mwajiri wako, shule yako au kampuni inayotoa huduma za barua-pepe kuhusu yaliyomo kwenye maandishi yako au juu ya mwenendo wako.
Tutahifadhi taarifa zako za kibinafsi katika mitambo yetu katika muda wote ule ambao unatumia huduma yetu uliyoiomba, na tunaweza kuziondoa wakati lengo litakapotekelezwa. Hata hivyo kwa sababu za kiusalama, Jarida la Mapishi inaweza kuhifadhi data za maandishi ya ujumbe (ikiwa ni pamoja na yaliyomo kwenye ujumbe, majina na wanachama, muda na tarehe) zilizotokana na matumizi ya huduma za jamii za Jarida la Mapishi (Jarida la Mapishi Community) kama vile Connector kwa muda wa miezi sita. Tutahakikisha kwamba taarifa za kibinafsi zilizotolewa zinahifadhiwa vizuri katika hali ya usalama, kulingana na Sheria ya Kulinda Data Binafsi ya mwaka 2023 (The Personal Data Protection Act 2023).
Kupata taarifa zako za kibinafsi
Una haki ya kuomba nakala ya taarifa zako za kibinafsi zinazokuhusu ambazo Jarida la Mapishi inazihifadhi na kusahihisha maelezo yoyote yenye makosa. (Tunatoza TZS 30,000) kwa maombi ya taarifa hizo.)
Watumiaji wenye umri wa miaka 16 au pungufu
Kama una umri wa miaka 16 au miaka pungufu ya hapo, tafadhali pata idhini kutoka kwa mzazi/mlezi wako wakati wote unapotaka kutoa maelezo yako kwenye mtandao wa Jarida la Mapishi. Watumiaji ambao hawana idhini ya aina hiyo hawaruhusiwi kutupatia taarifa zao za kibinafsi.