-
MaandaliziDakika 10
-
Kupika-
-
Walaji2
Smoothie ya blueberry na karanga, ni kinywaji kizuri kilicho sheheni Virutubisho vya Vitamini, Manganizi pamoja na Protini kwa wingi, ambacho chafaa kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Unaweza kunywa smoothie hii pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza smoothie hii ya blueberry na karanga.
Ingredients
Directions
Step1
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, maziwa, mtindi, matunda ya blueberry, ndizi, unga wa mbegu za kitani, siagi ya karanga, pamoja na asali, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Step2
Mimina smoothie kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Leave a Review