-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Sosi ya minti, ni sosi yenye ladha nzuri, ambayo hupikwa kwa kutumia majani ya minti, vitunguu maji, mtindi, limao, vitunguu vya kijani, pamoja na viungo vingine. Sosi hii yafaa kula pamoja na chakula chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya minti.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, vitunguu vya kijani, pamoja na vitunguu maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka majani ya giligilani, majani ya minti, pamoja na limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.
Weka garam masala, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa 12 mpaka 15.
Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, pamoja na chumvi, kisha koroga vizuri.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga. Weka maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review