-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Sosi ya nyanya na ukwaju, ni sosi yenye mchanganyiko wa ladha ya utamu na uchachu, ambayo inatokana na nyanya, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Sosi hii yafaa sana kula pamoja na wali au pamoja na chakula chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya nyanya na ukwaju.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka karanga kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Ondoa karanga hizo kwenye kikaango na uziweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye kikaango hicho hicho, nazi, mbegu za giligilani, 2 vijiko vya chai vya mbegu za binzari nyembamba, mbegu za mpopi, pamoja na mbegu za ufuta, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Ondoa mchanganyiko huo kwenye kikaango na uweke pembeni kwenye kontena lenye karanga, kisha acha vipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka binzari ya manjano, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, black seeds, ½ kijiko cha chai cha mbegu za binzari nyembamba zilizobaki, nyanya, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, chumvi, pamoja na mchanganyiko uliomo kwenye kontena, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa 10, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva.
Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka Tamarind Paste halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 30. Kumbuka kukoroga mara 1 au 2 wakati inachemka.
Epua sosi hiyo na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review